Nchini Peru, mradi wa Transformative Pathways unalenga katika kuimarisha mipango ya watu wa kiasili ya kulinda bioanuwai na kutawala maeneo yao katika maeneo ya Andean-Amazon. Hii inafanywa kupitia utumaji – na uwekaji kumbukumbu – wa mbinu za kitamaduni za kilimo cha Andean-Amazonia na mifumo ya utoaji inayotegemea eneo.
Washiriki wakuu katika mradi wa nchi hii ni Wampis katika maeneo ya Amazonas na Loreto (Amazon Kaskazini), watu wa Yanesha huko Pasco (Selva ya Kati), na watu wa Quechua huko Ayacucho.
Mradi huo nchini Peru unatekelezwa na mashirika mawili –Autonomous Territorial Government of The Wampis Nation (GTANW) na CHIRAPAQ – Centre of Indigenous Cultures of Peru. .
Dashed line
Shughuli
Maelezo Zaidi
Shughuli Muhimu
- Kusaidia ufuatiliaji wa kijamii na mifumo ya utawala wa eneo la jumuiya
- Kuzalisha upya bioanuwai na kuimarisha uhuru wa chakula cha jumuiya, riziki na kazi za kitamaduni.
- Utumiaji wa mbinu za kilimo cha Andean-Amazonian, ikijumuisha upandaji miti upya na urejeshaji wa wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka.
- Tafiti na mikakati ya kuandaa mifumo ya utoaji wa chakula, maji, riziki na udhibiti wa taka kulingana na eneo.
- Kushirikishana maarifa baina ya vizazi, elimu ya vijana wa kiasili kuhusu ulinzi wa maarifa asilia, eneo na kukabiliana na changamoto za sasa za kijamii na ikolojia.
- Utetezi na midahalo ya ngazi ya kitaifa kuhusu sheria na mapendekezo yanayohusiana na bioanuai na maeneo ya jamii asilia.
- Kusaidia jamii za kiasili kuandika na kubadilishana uzoefu
- Kukuza ujumuishaji wa mipango inayoongozwa na jamii asilia katika CBD (kwa mfano michango kwa NBSAPs) na Intergovernmental Science-Policy Platform on Biodiversity and Ecosystem Services (IPBES)