Miongoni mwa watu wa Igorot, muziki wa jadi wa sauti ni maarufu sana.. Kama vile muziki wa ala za kitamaduni kama vile gongo, mianzi, na ngoma, muziki wa sauti ni njia ya watu wa Igorot kuwasiliana, kubadilishana mawazo, kusimulia habari na hadithi, na kufufua uhusiano wao kama jamii asilia.
Katika kuadhimisha mila za kiasili, Partners for Indigenous Knowledge Philippines (PIKP)) na Mt Cloud Bookshop walipanga ‘Gag-ay: Nyimbo, Hadithi, Lishe’ tarehe 9 Agosti, 2025, kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya jamii asilia Duniani.
Tukio hili lilikuwa ni uzinduzi wa ‘Menday-eng Tako: Kitabu cha Vitabu vya Nyimbo za Jadi za Wenyeji wa Cordillera’. Kitabu hiki cha chap kinalenga kutoa vizazi vya sasa na vijavyo vya watu wa Igorot muhtasari wa nyimbo za kitamaduni katika majimbo sita ya Cordillera: ni nini madhumuni ya nyimbo hizi katika maisha ya ili, nyimbo hizi zinapaswa kuimbwa vipi, na jinsi gani mazoea haya ya kuimba bado yanafaa katika maisha ya kijamii ya Waigorot katika nyakati za kisasa?
Kupitisha Wimbo: Mabadilishano ya vizazi
Kitabu hiki ni matokeo ya ubadilishanaji wa nyimbo za kitamaduni za wazee na vijana kuhusu nyimbo za kitamaduni za Cordillera uliofanyika katika Jiji la Baguio mnamo Novemba 2022, ulioandaliwa na PIKP pamoja na Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Jimbo la Benguet (BSU CCA), Dap-ayan ti Kultura iti Kordilyera (DKK), na Kituo cha Vijana cha Cordillera (CYC).
Rasilimali za warsha hii walikuwa wazee na washika tamaduni wanaotoka Apayao, Benguet, Kalinga, na Mkoa wa Mlimani, wakati washiriki walikuwa vijana wa jamii asilia wa asili tofauti wanaoishi katika Jiji la Baguio na manispaa za karibu za Benguet. Kuelekea mwisho wa warsha, washiriki waliwasilisha matoleo yao ya nyimbo za kitamaduni zinazoakisi maslahi na mitazamo yao kama vijana wa mjini wa Igorot. Baada ya warsha, kazi ya shambani na mahojiano pia yalifanyika ili kujaza taarifa zaidi kuhusu nyimbo za kitamaduni za Cordillera.
Kutoka Wimbo hadi Lishe: Kuheshimu Mila ya Chakula
Kufuatia kipindi cha nyimbo za kitamaduni katika hafla ya Gag-ay, kulikuwa na mjadala juu ya mila ya vyakula vya Cordillera na onyesho la chakula jinsi ya kutengeneza linnapet – vitafunio vya wali (kichocheo kinaweza kupatikana kwenye tovuti ya PIKP).
Kupitia kujifunza kuhusu mifumo ya vyakula vya Asilia ya Cordillera, washiriki wa hafla hutafakari juu ya maadili ya kiasili ambayo yamepachikwa ndani yake:
Kutunza Ardhi
Jamii asilia hupata chakula chao kutoka sehemu zote za mazingira yao, kutoka kwa mashamba ya mpunga, bustani, misitu na maji. Kwa hivyo wanabeba jukumu la kulinda mazingira kama chanzo cha chakula, na cha maisha. Inaaminika kuwa ardhi na rasilimali zake zinapaswa kusimamiwa vyema, sio tu kwa kizazi cha sasa bali kwa vizazi vijavyo.
Uhisiano na jamii
Ushirikiano wa jamii unadhihirika katika mazoea ya uzalishaji wa kilimo, na vile vile katika kuandaa na kugawana chakula. Haya kwa kawaida hufanywa kupitia kazi ya pamoja, ambapo wanajamii hubadilishana katika kusaidiana. Hii inatufundisha kuthamini chakula cha asili ambacho ni cha afya, safi, na kinafaa kwa ajili ya kuhudumia familia na kushiriki na jamii.
Heshima kwa Ghaibu
Uhusiano wa kiroho kati ya jamii asilia umekuza mila na desturi zinazoheshimu na kulinda maeneo yao matakatifu na mazingira ya kuishi. Mzunguko mzima wa kilimo, hasa kabla ya kuanza kwa msimu wa kupanda na baada ya kuvuna, huwekwa alama ya siku za mapumziko, mila na karamu za jamii ambapo wanyama hutolewa, na nyama inashirikiwa na wote.